Monday, October 27, 2014

CHEKI DOGO ANAVYOPIGA PANCHI, KAMA TYSON

ENJOY NA VIDEO YA WAGOSI WA KAYA WAJA KIVINGINE

*LULU AACHIA FILAM YAKE MPYA YA MAPENZI YA MUNGU, IPATE SOKONI SASA

 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.
 Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.

Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.

Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa...
"Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"

Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.

Tuesday, September 9, 2014

*RAIS KIKWETE AHITIMISHA MAZUNGUMZO YAKE NA UJUMBE WA KITUO CHA DEMOKRASIA IKULU NDOGO DODOMA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana. Picha na IKULU

WATANO WAFIKISHWA KIZIMBANI KWA WIZI WA GARI LA IKULU KENYA

WATU watano akiwemo raia mmoja wa Uganda pamoja na fundi mmoja wa magari wameshitakiwa kwa kosa la wizi wa gari la msafara wa ulinzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Kenya. 
Watu hao pia walishitakiwa kwa kumuibia gari inspekta wa polisi David Machui, aliyekuwa akiendesha gari hilo aina ya BMW 735 mnamo Agosti 26 mjini Nairobi lilipoibwa. 
Washukiwa hao wote walikanusha madai hayo kwamba walihusika katika wizi wa gari hilo. Kila mshukiwa aliachiliwa kwa kima cha shilingi milioni 5 isipokuwa mwanamume mmoja aliyesemekana kuwa na kesi tofauti mahakamani. 
Raia wa Uganda Robert Mande Ochan, aliamrishwa na mahakama kutoa dhamana ya shilingi milioni mbili ili aweze kuachiliwa. Gari hilo lilipatikana mjini Kampala Uganda na kurejeshwa nchini Kenya siku ya Ijumaa. 
Washukiwa hao walioiba gari hilo wakiwa wamejihami, wanashukiwa kuwa sehemu ya mtandao wa wezi wa magari wakiendeshea kazi yao nchini Kenya, Burundi, DRC , Tanzania na Uganda. 
Kikundi hicho kiko na wahalifu, maafisa wafisadi wa kutoza ushuru na mafundi wa magari. Polisiwa wa Uganda walipata hari hilo baada ya mpenzi wa mshukiwa mmoja kumuwekea mtego ambao ulimfikisha kwa polisi, katika mtaa wa Wandegeya, mjini Kampala. 
Maswali yamekuwa yakiulizwa kuhusu afisaa wa polisi aliyeruhusiwa kuendesha gari la serikali kama gari lake binafsi, wakati utaratibu unasema kuwa magari yote ya serikali yanapaswa kuegeshwa katika kituo cha polisi kilicho karibu na dereva wa gari hilo.